Thursday 18 May 2017

Huku kukiwa na uwezekano mkubwa kwa kipa David de Gea kutua Real Madrid majira haya ya joto, mlinda mlango huyo angeweza kucheza mechi ya kuagwa Manchester United, lakini hilo halitawezekana tena.
Uamuzi huo umetokana na Jose Mourinho kueleza kuwa makipa Kieran O’Hara, Sergio Romero na Joel Pereira ndiyo watakaocheza mechi zilizosalia ikiwamo ya jana dhidi ya Southampton.
Hofu kubwa kwa mustakabali wa baadaye wa De Gea kwa United ni wakati huu Real Madrid ikijiandaa kutoa ofa zaidi ya pauni milioni 60 kwa kipa huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 26.
Tayari Mourinho amethibitisha kuwa Romero atacheza mechi ya fainali ya Europa League dhidi ya Ajax.
Kocha huyo wa United pia aliahidi kumpa nafasi ya kuanza na kucheza kwa dakika zote kipa namba tatu, Pereira, 20, na anajipanga sasa kuivaa Crystal
Palace Jumapili.
Inaelezwa kuwa inaonekana kama De Gea si mwenye furaha kwa maamuzi hayo ya Mourinho ya kumpa nafasi Romero kucheza mechi ya fainali ya Europa League.

Mhispania huyo pia anaamini amekosa matumaini kutokana na uchezaji mbaya wa safu ya ulinzi wakati wakiangukia pua dhidi ya Arsenal na Tottenham, baada ya Mourinho kupoteza mbio za kumaliza nne-bora.

No comments:

Post a Comment