Tuesday 30 May 2017

Mwita Waitara:Asilimia kubwa ya majibu Mawaziri ni uongo


Mwita Waitara Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) leo aliwashambulia mawaziri wa Rais Magufuli kwa kueleza kuwa majibu yao asilimia kubwa ni ya uongo,
Mwita ameelekeza mashambulizi hayo leo bungeni wakati alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kudai kuwa majibu yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliani, Isack Kamwelwe ni asilimia tano tu ya swali lake na asilimia 95 ni uongo.
“Mimi ni mwalimu wa hisabati na kemia nimekuwa nisahihisha mitiani ya serikali na kama ningekuwa nasahisha mitihani ya mawaziri wewe ningekupa asilimia tano tu kati ya mia majibu niliyouliza imejibiwa asilimia tano tu yaliyobaki ni uongo.
“Inaonesha waziri hauna taarifa sahihi ya miradi ya maji ya kata nilizozitaja katika swali la msingi Je, huko tayari sasa uniletee taarifa sahihi.
“Je, kwa sasa hupo tayari nikukutanishe na akina mama ambao wanakumbana na adha ya kutafuta maji na kulazimika kununua maji kwa sh. 500 kwa ndoo ili uweze kusikiliza kilio chao juu ya kukosekana kwa maji?” alihoji Waitara katika swali lake la nyongeza.
Awali katika swali la msingi Waitara alitaka kujua serikali itakamilisha lini miradi ya maji ya kata za Chanika, Kipunguni na Majohe ili wananchi wa kata hizo na maeneo ya jirani wapate maji ya uhakika.



Pia mbunge huo alitaka kujua ni lini serikali itachimba bwawa kubwa katika mnada wa kimataifa ili ng’ombe wanaouzwa ili wapate maji.
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Isack Kamwelwe, amesema serikali inakamilisha miradi ya maji ya kata za Chanika, Kipunguni na Majohe.
Amesema miradi mingi imekamilika na inawahudumia wananchi na mingine hipo katika hatua nyingine za ujenzi, miradi iliyokamilika ni pamoja na Kipungunguni ‘B’ kwa Mkoremba, Chanika shuleni, Majohe, Nyang’andu na Msongola.
Kamwelwe amesema serikali imepanga kupeleka maji katika maeneo ya Pugu kutoka katika miradi mkubwa wa visima virefu vilivyopo mpera katika wilaya ya Mkuranga na kazi ya uchimbaji wa visima inaendelea na matarajio ya kukamilisha uchimbaji katika mwaka huu wa fedha.
Mbunge awashambulia mawaziri wa Rais Magufuli

No comments:

Post a Comment