Wednesday 17 May 2017

Watakao vunja Sheria za Huduma za Treni za Abiria kutupwa Jela Miezi 6

Meneja huduma za wasafiri TRL, Iddi Mzugu
Watumiaji wa huduma za usafiri wa treni za abiria za Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wametakiwa kuzingatia sheria za matumizi ya usafiri ili kuepuka adhabu ya kufungwa jela miezi sita.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam  Meneja Huduma za Wasafiri TRL, Iddi S. Mzugu amesema kuwa matumizi ya usafiri wa abiria unasimamiwa na sheria, kanuni na taratibu kwa masharti maalum hivyo abiria hawapaswi kutodandia mabehewa baada ya milango kufungwa.
Ameeleza kuwa uongozi wa TRL unatoa rai kwa wananchi kutokufanya hivyo na endapo mtu akibainika amefanya hivyo kudandia mabehewa yakiwa yamefungwa atakamatwa na atafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo kisichopungua miezi sita jela.
Alifafanua kuwa abiria wamekuwa wakipoteza maisha kwa kufariki kutokana na kudandia mabehewa wakati tayari treni ikiwa imeondoka.

Wakati huohuo Kikosi cha Polisi Reli kimeanza operesheni ya kuwadhibiti abiria ambao hawafuati sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya usafiri salama wa Treni.                

No comments:

Post a Comment