Friday 19 May 2017

Wachezaji wanaojirusha makusudi kukiona chamoto

Wachezaji wa soka ni watu wajanja janja na wanajaribu kufanya kila namna wawezayo iwe sawa au sio sawa ili mradi kuzisaidia timu zao kuibuka kidedea.
Kati ya mambo yamekuwa yakiziumiza sana timu pinzani na mashabiki na matukio ya kutafuta faulu au penati kwa kujiangusha hata bila kuguswa(Dive)
Kudive limekuwa ni tatizo sio tu Epl bali dunia nzima, lakini chama cha soka cha Uingereza kimechoshwa na uongo huo na sasa wameamua kulivalia njuga.
Mchezaji yeyote ambaye atajaribu kumdanganya muamuzi kwa kujirusha au kutafuta kadi nyekundu kwa wapinzani au ya njano atapewa adhabu ya kufungiwa michezo miwili.
Sheria hiyo itaanza kutumika msimu ujao,matukio kama la Rashford dhidi ya Swansea,Kane dhidi ya Arsenal au Sane dhidi ya Middlesbrough yamekuwa gumzo sana kutokana na aina ya penati walizopewa.
Robert Snordgrass wa Hull City aliwahi kukiri kwamba penati waliyopewa dhidi ya Crystal Palace haikustahili kwani yeye alijaribu kukwepa kiatu na refa akaweka tuta.

Mchezaji atakayejirusha ataweza kumaliza mchezo lakini baadae FA kwa kushirikiana na kamati ya waamuzi watapitia tukio na kisha kutoa maamuzi kuhusu kesi husika.

No comments:

Post a Comment