Sunday 14 May 2017

Arsene Wenger: Mashabiki waandamane tu

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kwamba hatishwi na maandamaano yanayopangwa na mashabiki wa klabu hiyo ili kumpiga.
Wenger alisema hana hofu kwani yeye siyo mwanasiasa, bali amejikita kwenye soka zaidi.
Klabu hiyo jana Jumamosi, iliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Stoke City waliokuwa nyumbani.
Ushindi huo umewapa matumaini makubwa ya kufuzu mashindano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao, baada ya Oliver Giroud kuziona nyavu mara mbili na washambuliaji Mesut Ozil na Alex Sanchez kufunga bao moja kila mmoja.

No comments:

Post a Comment