Wednesday 31 May 2017

Niko tayari kuondoka Barcelona- Iniesta

Nohodha wa Barcelona, Andres Iniesta bado ana ndoto za kuzeekea kwenye Liga ya La Liga, huku akisema kwamba iwapo atatakiwa kuondoka yupo tayari kufanya hivyo.
Iniesta mwenye miaka 33 mkataba wake unamalizika katikati ya mwaka 2018 na hatima yake imebaki njiapanda. Msimu huu alianza mechi 13 za ligi msimu huu.
Kiungo huyo alisema bado ndoto zake ni kustaafu maisha ya soka akiwa kwenye klabu yake ya Barcelona ambayo alijiunga  tangu akiwa na miaka 12, akichezea timu ya vijana.

No comments:

Post a Comment