Thursday 18 May 2017

Serengeti Boys kuikabili Angola leo

. Timu ya soka ya vijana ya Taifa leo Alhamisi inatarajiwa kukata kiu ya Watanzania kwenye mchezo wake wa pili katika mashindano ya Afrika.
Mchezo wa kwanza, Serengeti Boys iliishangaza Mali baada ya kutoka suluhu ya 0-0.
Timu hiyo mpaka sasa imefikisha pointi moja na matokeo mazuri ya leo inaweza kuifanya kusogea hadi nafasi ya kwanza kwenye kundi B.
Macho na masikio ya Watanzania yataelekezwa kwenye runinga zao, huku wakiiombea dua ili iweze kushinda ili kusonga mbele katika mashindano hayo yanayoendelea nchini Gabon
.

No comments:

Post a Comment