
Saudi Arabia imeanzisha mipango ya kujenga mji wa burudani kando mwa mji
wa Riyadh ambao utakuwa mkubwa mara 50 zaidi ya himaya ya Uingereza ya
Gibraltar.
Mji huo ambao utakuwa na ukubwa wa kilomita 334 mraba ambao utakuwa sawa
na mji wa Las Vegas, utatoa huduma za kitamaduni, michezo na mambo
mengine ya burudani.
Inaripotiwa kuwa mji utakuwa wa aina yake duniani.
Ujenzi wa mji huo utataanza mapema mwaka ujao na awamu ya kwanza kukamilika mwaka 2022.
Katika malengo ya mwaka 2030 uliotangazwa na naibu mfalme Mohammad Bin
Salman mwaka mmoja ulipita, una lengo la kuboresha uchumi na kuzuia
kutegemea mafuta kwa taifa hilo.
Mji huo ambao ni kama sehemu moja ya tano ya mji wa Riyadh, ndio mradi wa hivi punde kutangazwa.
Utawala unasema kuwa matumaini ni kuwa utawavutia wageni, kuboresha
uchumi na ukawa wa burudani na furara kwa wale wataishi mji mkuu Riyadh.
No comments:
Post a Comment