Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wajumbe katika Baraza
la Saba la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS),
lililofanyika mkoani Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale ambaye ni Mwenyekiti
wa Baraza la Saba la Wafanyakazi akitoa taarifa ya utendaji kazi wa
Wakala huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa (hayupo pichani). Baraza hilo limefanyika mkoani Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la
Saba la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS),
wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa (hayupo pichani), katika Baraza hilo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (kushoto) akiteta
jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa katika Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala huo lililofanyika
mkoani Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na
wajumbe wa Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini
(TANROADS).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza mmoja wa wajumbe
waliohudhuria katika Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara
nchini (TANROADS), mkoani Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameagiza Wakala wa Barabara nchini
(TANROADS) kuboresha Idara ya Mipango na Usanifu katika wakala huo ili
kupata matokeo mazuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.
Prof. Mbarawa ameutaka wakala huo
kuboresha kanuni zinazosimamia aina ya vyombo vya moto vinavyotumia
barabara zote nchini ikiwemo ili kuweza kusaidia miundombinu hiyo kudumu
muda mrefu.
Akizungumza mkoani Dodoma katika
ufunguzi wa Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala huo Prof. Mbarawa
amesema kuwa wakala unabidi uanze kubadili aina ya mfumo wa usanifu
uliokuwa ukitumika awali na badala yake utumike usanifu wa kisasa
unaoendana na mahitaji halisi ya watumiaji wa barabara hizo.
“Kama mnaona kuna mabadiliko
yoyote mnayohitaji kuyafanya ili barabara zetu zidumu, boresheni kanuni
na mlete kwangu ili nizifanyie kazi”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza kuwa katika kuboresha
utendaji katika wakala huo, Serikali ina mpango wa kuwapa fursa za ajira
wahandisi hususani wanawake ili na kuwajengea uwezo na kuweka uwiano
katika taalamu hiyo.
Aidha Waziri Prof. Mbarawa
ameahidi kuongeza fedha za uendeshaji kwa wakala huo ili kuuwezesha
kutekeleza miradi mbalimbali inayoendelea nchini.
“Kumbukeni majukumu ya Wakala
yameongezeka sasa hamtajenga barabara pekee, mmeongezewa jukumu la
kujenga miundombinu ya viwanja vya ndege hivyo ni muhimu kujipanga
kutekeleza kazi hii”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye, Mtendaji Mkuu wa TANROADS,
Eng. Patrick Mfugale ameahidi kushughulikia ujenzi wa viwanja vya ndege
ikiwemo kufanya kazi kwa weledi na uadilifu kama ambavyo wakala huo
unatekeleza miradi yake ya barabara
Ameongeza kuwa Wakala unaendelea
kufanya kazi na Makandarasi wenye uwezo na wanaozingatia thamani ya
fedha katika miradi yote inayotekelezwa nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi
ya TANROADS, Eng. Hawa Mmanga amemuahidi Waziri Prof. Mbarawa kufanya
kazi kwa uadilifu, bidii, na kuzingatia thamani ya fedha katika miradi
yote inayotekelezwa na wakala.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment