Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akiwa kwenye studio za
televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) visiwani Zanzibar
kutoa elimu ya mpiga kura juzi.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akifafanua jambo kwenye
studio za televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) visiwani
Zanzibar wakati akitoa elimu ya mpiga kura juzi.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akifafanua jambo kwenye
studio za televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) visiwani
Zanzibar wakati akitoa elimu ya mpiga kura juzi.Kushoto ni muandaaji wa
vipindi wa ZBC, Salha Mohamed akiongoza kipindi cha Alasiri Yetu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani, akisalimiana na
Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Iman Osmond (katikati) na Naibu MkurUgenzi Mkuu
wa Shirika hilo Nasra Mohamed baada ya kumaliza kipindi cha Alasiri
Yetu, kutoa elimu ya mpiga kura.
Picha na Hussein Makame,NEC
Hussein Makame, NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
inatarajia kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura ifikapo mwaka wa
fedha wa 2017/2018 kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi mkuu uliopita wa
mwaka 2015.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani wakati akitoa elimu ya mpiga kura
kupitia kipindi cha Alasiri Yetu kinachorushwa na televisheni ya Shirika
la Utangazaji Zanzibar (ZBC).
Alisema kuwa baada ya uboreshaji
huo wa mwaka 2017/2018, Tume hiyo inategemea kuboresha kwa mara ya pili
daftari hilo ifikapo mwaka wa fedha 2019/2020.
Bw. Kailima alifafanua kuwa
uboreshaji huo unafanyika kwa mujibu wa kifungu namba 5 cha Sheria ya
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinachoielekeza NEC kuboresha daftari hilo
mara mbili.
“Kwa mujibu wa kifungu namba 5
cha Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinasema Tume ya Taifa ya
Uchaguzi itapaswa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura mara mbili,
baada ya uchaguzi mara moja na kabla ya uchaguzi ujao mara moja”
alisema Bw. Kailima na kuongeza kuwa:
“Kwa hiyo tumemaliza uchaguzi
mwaka jana na kabla ya uchaguzi wa mwaka 2020, Mungu akituweka hai
tunategemea mwaka 2017/2018 tuboreshe daftari na mwaka 2019/2020 tufanye
hivyo”
Mbali na kuzungumzia uboreshaji
wa daftari la kudumu la wapiga kura, Bw. Kailima aleleza jinsi tume hiyo
inavyotekeleza mikakati ya kutoa elimu ya mpiga kura na kwamba NEC
itajipanga ili kwenda kutoa elimu hiyo visiwani Zanzibar.
Alisema NEC inapanga kwenda kutoa
elimu hiyo kwenye Chuo Kikuu Zanzibar (State University) mjini Unguja
na baadaye kwenda kisiwani Pemba na pia inategemea kushiriki Jitimai ili
kutoa elimu ya mpiga kura kwa washiriki wa mjumuiko huo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
inaboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa lengo la kuandikisha
kila raia mwenye sifa za kupiga kura na kutunza taarifa zake katika
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Inaelezwa kuwa kuwepo kwa Daftari
sahihi la Wapiga Kura linaloaminiwa na wadau ni kigezo muhimu cha
kufanikisha chaguzi huru, wazi, zenye kukubalika na za haki zaidi.
No comments:
Post a Comment