Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt
Kebwe Stephen Kebwe akipokewa na mkuu wa kitengo cha Kuboresha
usalama wa jamii ( DCP) Godluck Mongi alipokwenda kufungua mafunzo ya
upelelezi kwa askari wa polisi 100. ( katika ni Mkuu wa mafunzo wa Jeshi
la Polisi DCP Ally Lugendo. Mafunzo hayo yanafanyika katika chuo cha
polisi kidatu yamefadhiliwa na Taasisi ya Hanns Sidel.
Picha na Tamimu adam- Jeshi la Polisi.
Na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe
Stephen Kebwe amefungua mafunzo ya upelelezi kwa askari 100 kutoka mkoa
wa kipolisi kinondoni, mkoa ambao Jeshi la polisi nchini limeuchangua
kuwa eneo la mfano katika kutekeleza mpango wa kuboresha usalama wa
jamii uliozinduliwa katika viwanja vya Biafra kinondoni jijini Dar es
salaam.
Mafunzo hayo ya upelelezi ya
miezi miwili yamefunguliwa katika chuo cha maafisa wa Polisi kidatu
kilichopo mkoani morogoro yamefadhiliwa na taasisi ya isiyokuwa ya
kiserikali ya Hanns Sidel inayotekeleza miradi mbalimbali hapa nchini.
Akifungua mafunzo hayo mkuu wa
mkoa huo, Dkt Kebwe alisema kuwa amefurahishwa na kitendo cha cha Jeshi
la Polisi kuamua kuchangua mkoa wa Morogoro kufanyia mafunzo hayo na
pia kumchagua yeye kuwa mgeni rasmi.
Dkt Kabwe alilipongeza Jeshi la
Polisi kwa kazi ngumu wanayoifanya ya kuimarisha usalama wa raia na mali
zao na aliwataka askari wanaopata mafunzo hayo katika chuo cha maafisa
wa polisi kidatu kutumia weledi na taaluma hiyo watakayoipta kutatua
kero za wananchi zinazotokana na ucheleweshaji wa upelelezi .
“ Nimefurahi sana kusikia kuwa
mafunzo haya yanalenga kuharakisha upelelezi na kesi yoyote itakuwa
inapelelezwa itakuwa imekamilika ndani ya siku sitini” alisema Dkt
Kebwe.
Mapema akitoa utangulizi wa
mafunzo hayo, mkuu wa kitengo cha kinachoratibu utekelezwaji wa mpango
wa Jeshi la Polisi wa kuboresha usalama wa jamii, Naibu Kamishina wa
Polisi (DCP) Godluck Mongi alisema kuwa mafunzo hayo ya upelelezi
yataleta mafanikio makubwa katika mkoa huo wa kinondoni kwa kuharakisha
upelelezi wa kesi .
Aliongeza kuwa lengo la maboresho
hayo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2019 askari wote upelelezi wawe
wamepata mafunzo hayo na hatimaye kupuza kero ya uhalifu katika mkoa wa
kinondoni kwa asilimia 10%
Naye mwakilishi wa Taasisi
inayofadhili mafunzo hayo, Bw. Ombeni mhina alisema kuwa ufadhili wa
mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi 100 kutoka mkoa wa kipolisi
kinondoni ni sehemu ya mpango wa Taasisi ya Hanns Seidel kuunga mkono
jitihata za jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kwa raia
na mali zao kupitia mpango wa kuboresha usalama wa jamii unaoendelea
kutekelezwa katika mkoa wa kipolisi kinondoni.
Aliongeza kuwa Tanzania ni
miongoni mwa nchi sitini ambazo jumla ya miradi 100 inaendelea
kutekelezwa ikiwa na lengo la kukuza demokrasia, amani na maendeleo
duniani kote.
Kwa upande wake mkuu wa chuo
cha Polisi Kidatu kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrea Mwang’onda
aliwataka wanafunzi wanaopata mafunzo hayo ya upelelezi kuzingatia kile
wanachofundishwa na kufuata maadili yote ya uaskari wakati wote
watakapokuwa katika mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment