
Msanii mkongwe Zahir Ally Zorro alikuwepo kutoa burudani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Jumanne hii alimwandalia dhifa ya Taifa, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo (DRC) Joseph Kabila Ikulu jijini Dar es salaam.
Shughuli hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mkali wa masauti Christian Bella alikuwa mmoja kati ya wasanii ambao walialikwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kusherehesha shughuli hiyo.




Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akimtuza mwanamuziki
Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa “Nani kama Mama” kwenye
dhifa hiyo

Mama Janeth Magufuli akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa “Nani kama Mama” kwenye dhifa hiyo


Mama Salma Kikwete akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa “Nani kama Mama” kwenye dhifa hiyo

Spika Mstaafu Mhe Anne makinda akimtuza mwanamuziki Christian Bella
kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa “Nani kama Mama” kwenye dhifa hiyo



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na
mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila
wakiagana na viongozi wastaafu Ikulu jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment