Naibu Katibu Mkuu wa klabu ya
gofu ya Lugalo ya Jijini Dar es Salaam Kanali Rajabu Mwenyumbu
akiangalia Mazoezi ya mwisho ya timu ya klabu hiyo ambayo inatarajia
kushiriki katika mashindano ya wazi yanayotarajia kufanyika
Mwishoni mwa Wiki Hii Jijini Arusha. (PICHA NA LUTENI SELEMANI
SEMUNYU)
Naibu katibu mkuu wa Klabu ya
Gofu ya Jeshi ya Lugalo Kanali Rajabu Mwenyumbu akisalimiana na
wachezaji wa gofu wa timu hiyo wanao tarajiwa kushiriki katika
mashindano ya wazi Jijini Arusha mwisho wa Wiki hii. PICHA NA LUTENI
SELEMANI SEMUNYU)
Naibu katibu mkuu wa Klabu ya
gofu ya jeshi ya Lugalo Kanali Rajabu Mwenyumbu akizungumza na
wachezaji wa gofu wa klabu hiyo ya jijini Dar es salaam wanao tarajiwa
kushiriki katika mashindano ya wazi yanayotarajia kufanyika mwisho wa
Wiki hii Jijini Arusha .(PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)
Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ
TIMU
ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo imetamba
kuendeleza ushindi katika mashindano ya wazi ya Mchezo wa golf
yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi Oktoba 15 na 16 Jijini Arusha kwa
kurejea na Ushindi.
Hayo
yamesemwa na Naibu katibu mkuu wa Klabu hiyo Kanali Rajabu Mwenyumbu
wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwa Niaba ya mwenyekiti wa
Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo wakati akiaga Timu hiyo
katika Uwanja wa Golf wa Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Kanali Mwenyembu alisema maandalizi mazuri yamefanyika kwa Timu zote ambazo zitashiriki mashindano hayo ambazo ni Daraja Senior ,A,B,C na Wanawake na watoto na kila daraja liko Vizuri na matumaini ni makubwa.
“Nataka
muendeleze nidhamu ya Kijeshi katika Michezo lakini weledi katika
mashindano ili kuhakikisha wanarejea na ushindi badala ya kuwa washiriki
katika mashindano hayo ambayo ni muhimu kwa viwango vya Wachezaji” Alisema kanali Mwenyumbu.
Kwa Upande wake Mmoja
wa Wachezaji hao Sara Damas Alisema ni matumaini yake kuwa licha ya
kuibuka na ushindi lakini pia wanatarajia kupanda viwango vya uchezaji
ukilinganisha na wakati uliopita.
Naye Mchezaji Juma Likuli
alisema mazoezi yaliyofanyika ni tofauti zaidi yaliyowajenga ipasavyo
hali inayowapa matumaini makubwa ya kuibuka ushindi.
Kwa upande wake Nahodha wa Klabu hiyo Kapteni Japhet Masai alisema Jumla ya wachezaji 10 wanatarajiwa kwenda kushiriki michuano hiyo wakiwemo wanawake watatu na wanaume Saba.
Aliongeza kuwa kikosi cha wachezaji hao Kitaongozwa na Kapteni Amanzi
Mangengule, Kapteni Japhet Masai, Kapteni Kibuna Shabani, Juma
Likuli,Noel Mheni,Nicolous Chitanda ,Michael Obare, Amina Hamisi,Sara
Denis na Sophia Mathias.
Kapten
Masai aliongeza kuwa maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni
kurejea na Ushindi kama ilivyokuwa katika mashindano yaliyopita ya
Tanzania Open,Moshi Open na CDF Trophy ambayo klabu ya Lugalo iliibuka
washindi.
No comments:
Post a Comment