Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiwasilisha mada ya
masuala ya Watu wenye Ulemavu wakati wa mkutano wa wadau wa masuala hayo
walipowasilisha Matokeo ya Tafiti Mpya ya Ubainishaji Hali Halisi ya
Ulemavu na Uzee Nchini uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano hoteli ya
Serena Dar es Salaam Oktoba 12, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkalimani wa lugha ya alama
Bw.Thomas Shayo akifasiri ujumbe kwa kundi la watu wenye ulemavu
(wasiosikia) uliotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano
wa wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum uliofanyika katika
Ukiumbi wa hoteli ya Serena Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Mtafiti Rika Shirikisho la Watu
wenye Ulemavu Bi. Regina Mbaji akiwasilisha mada wakati mkutano wa wadau
wa masuala la watu wenye mahitaji maalum walipowasilisha matokeo ya
tafiti Mpya ya Ubainishaji Hali Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini Ukumbi
wa Mikutano hoteli ya Serena Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Mshiriki Rika (kundi la wazee)
Bi.Elizabeth Nkwera akitoa mada ya usawa wa huduma za kijamii kwa
makundi maalum wakati wa Mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye
mahitaji maalum walipowasilisha matokeo ya tafiti Mpya ya Ubainishaji
Hali Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na baadhi ya
wadau walioshiriki katika Mkutano wa kujadili masuala ya watu wenye
mahitaji maalum uliofanyika katika hoteli ya Serena Oktoba 12, 2016, wa
kwanza kulia ni Bi. Clotilda Isdori na katikati ni Bw.Elisha Sibale.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wadau wa masuala la
watu wenye mahitaji maalum ulioandaliwa na Mashirika ya misaada. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment