Baadhi ya vijana wakijibu maswali
mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na Maofisa wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi –NEC (Kulia) waliokuwa wakitoa Elimu ya Mpiga Kura wakati wa
maadhimisho ya Wiki ya Vijana mkoani, wilayani Bariadi, Simiyu. Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaendelea kutoa Elimu ya Mpiga kura nchini kwa
kukutana na wananchi wa makundi mbalimbali.
Afisa kutoka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Bw. Hubert Kiata akitoa elimu ya Mpiga kura kwa wakazi wa
wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya
Vijana.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya
Bariadi waliojitokeza kupata Elimu ya Mpiga Kura iliyokuwa ikitolewa na
Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mkoani Simiyu. Tume ya Taifa
ya Uchaguzi imeanzisha programu endelevu za kuwafikia wananchi moja kwa
moja kuwapatia elimu ya mpiga kura kupitia mikutano, maonesho mbalimbali
na vyombo vya habari.

Maofisa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) Bw. Hurbert Kiata (kulia) na Upendo wakisikiliza kwa makini Hoja
na maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na vijana wa wilaya ya
Bariadi kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Taratibu na Sheria zinazosimia
Chaguzi za Tanzania.
Picha / Aron Msigwa –NEC.
No comments:
Post a Comment