Mkurugenzi wa Idara ya Habari,
MAELEZO Bw. Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu taasisi za Serikali kutekeleza agizo la kuhuisha taarifa
na huduma katika Tovuti zao mapema kabla ya mwisho wa mwezi huu katika
mkutano uliofanyika Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao (EGA) leo Jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa
Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto.
Meneja wa Habari, Elimu na
Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi
hao leo jijini Dar es Salaam, kuhusu taasisi za umma kuhuisha taarifa
katika Tovuti zao. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw.
Hassan Abbas.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari,
MAELEZO Bw. Hassan Abbas akiwaonyesha waandishi wa habari mwongozo wa
utengenezaji wa Tovuti za Serikali wakati wa mkutano wake na waandishi
hao leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Habari, Elimu na
Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia mkutano wao na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw.
Hassan Abbas na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala wa
Serikali Mtandao (EGA) Bibi. Suzan Mshakangoto (hawapo pichani). Mkutano
huo ulihusu kuzikumbusha Taasisi za umma kuhuisha taarifa katika Tovuti
zao leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari,
MAELEZO Bw. Hassan Abbas akielezea namna ambazo mitandao ya kijamii
inavyo tumika kurahisisha kufikisha taarifa za Serikali kwa jamii na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu taasisi za umma leo Jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala
ya Serikali Mtandao, Bibi. Susan Mshakangoto. Mkurugenzi huyo alitolea
mfano wa akaunti ya Tweeter ya, Msemaji wa Serikali@ TZ_Msemaji Mkuu.
Mwananchi anaweza kuifuata akaunti hiyo kwa kutafuta “Msemaji Mkuu wa
Serikali on Twitter”.
Picha na: Frank Shija, MAELEZO
No comments:
Post a Comment