Snura akizungumza na waandishi wa habari
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
amemruhusu msanii wa muziki, Snura Anthony Mushi ‘Snura’ kuachia video
yake mpya ya wimbo ‘Chura’ baada ya msanii huyo kufanya marekebisho ya
video ya wimbo huo na kukubaliwa na wizara.
Aidha, katika barua ya wizara imemtaka Snura kuomba radhi mbele ya waandishi wa habari ili video hiyo ianze kuchezwa.
Mapema mwaka huu video ya wimbo huo ulitangazwa kufungiwa na serikali baada ya video hiyo kukosa maadili ya kitanzania.
Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Maisha Basement jijini
Dar es salaam, Snura amesema anamshukuru Mh waziri Nape Moses Nnauye kwa
kumkubalia ombi lake la kuiruhusu kazi hiyo kutoka.
“Mh Nape ameuruhusu wimbo wangu mpya wa Chura na video Chura kupigwa na
kuonyeshwa katika vituo mbali mbali vya radio na runinga baada ya kuona
video yangu mpya ya wimbo ina maadili na ujumbe ndani yake ikiwa ni
kukidhi makubaliano ya awali kwamba wimbo wangu ‘Chura’ utakafunguliwa
pale nitakapofanya video mpya ya muziki yenye maadili ya kitanzania,”
alisema Snura.
Aliongeza, “Video yangu mpya Chura inaeleza maana halisi ya neno Chura.
Chura ninae mzungumzia ni mwanamke anaeruka ruka katika mahusiano kwa
kubadilisha wanaume mbalimbali matokeo yake kupata magonjwa sugu,”.
Pia katika barua hiyo ya Mh Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye amempa onyo kali msanii huyo kutokurudia kufanya
tena video zisiyokuwa na maadili ya kitanzania.
No comments:
Post a Comment