Monday, 19 September 2016

Ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni Loliondo Wilayani Ngorongoro

1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni akipokea maelezo kutoka kwa Afisa Ardhi na Maliasili wa Wilaya ya Ngorongoro Bw.Sixsbert Byorusheng  kuhusu mpaka wa Tanzania na Kenya uliopo kijiji cha Olaika, Loliondo Wilayani Ngorongoro wakati wa ziara yake ya kukagua usalama wa mipaka ya nchi ambapo Idara ya Uhamiaji inatarajia kujenga kituo ili kudhibiti usalama na mapato ya sereikali katika eneo hilo.
2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni akiangalia kwa kutumia darubini mpaka wa Tanzania na Kenya uliopo kijiji cha Olaika, Loliondo Wilayani Ngorongoro wakati wa ziara yake ya kukagua usalama wa mipaka ya nchi. Idara ya Uhamiaji inatarajia kujenga kituo ili kudhibiti usalama na mapato ya sereikali katika eneo hilo.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Rashid Taka
3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni  akizungumza na wakazi wa kata ya Soitisambu,Tarafa ya  Loliondo Wilayani Ngorongoro wakati wa ziara yake ya kukagua usalama wa mipaka ya nchi wilayani humo ambapo Idara ya Uhamiaji inatarajia kujenga kituo ili kudhibiti usalama na mapato ya sereikali katika eneo hilo.
4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakazi wa kata ya Soitisambu,Tarafa ya  Loliondo Wilayani Ngorongoro wakati wa ziara yake ya kukagua usalama wa mipaka ya nchi wilayani humo ambapo Idara ya Uhamiaji inatarajia kujenga kituo ili kudhibiti usalama na mapato ya sereikali katika eneo hilo.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).

No comments:

Post a Comment