
Usalama mkali umedumishwa nchini Saudi Arabia
Takriban Mahujaji wa kiislamu milioni 1.5 wamekusanyika nchini Saudi
Arabia chini ya ulinzi mkali, kabla ya kuanza rasmi ibada ya hija ya
kila mwaka.
Magari yamepigwa marufuku ya kukaribia msikiti mkuu, Grand Mosque, ambao
ni eneo takatifu zaidi kwa waislamu, huku mahujaji wakifanyiwa ukaguzi
na polisi katika vituo kadhaa kwenye eneo hilo.
Hija hii ni moja ya mikutano mikubwa zaidi ya kidini duniani
Zaidi ya mahujaji 2000 waliaga dunia mwaka jana wakati wa ibada ya hija, wengi wao wakiwa raia wa Iran.Iran iliilaumu Saudi Arabia kwa kutosimamia ibada za Hija inavyofaa, na imekataa kuwaruhusu raia wake kuenda Saudi Arabia kuadhimisha ibada ya Hija.

No comments:
Post a Comment