
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa anafanya sana media tour kwenye nchi nyingine kwakuwa inamsaidia kupata mashabiki wengi zaidi.
“Unajua nafanya sana media tour, kwani wenzetu ni wazito sana kupokea kazi za wasanii wa nje ya kwao. Hivyo hizo media tour zinanisaidia kujenga fan base katika nchi zao,” amesema Vee.
Vee Money ni mmoja kati ya wasanii wachache wa Bongo Fleva waliofanikiwa kupata collabo na wasanii wa nje akiwa tayari ameshafanya kazi na wasanii kutoka nchi tofauti topfauti ikiwemo Nigeria, Togo, Malawi, Ufaransa na sehemu zingine.
No comments:
Post a Comment