Serena Williams atupwa nje kwenye michuano ya US Open
Serena Williams ameendelea kuharibu kwenye mashindano ya tennis baada
ya hapo jana kuondolewa kwenye nusu fainali ya michuano ya US Open na
mchezaji wa Jamhuri ya Czech, Karolina Pliskova.
Kwenye mchezo huo Karolina alifanikiwa kushinda kwa seti 6-2, 7-6 (3)
katika mchezo uliofanyika kwa muda wa saa moja na dakika 26. Kwa sasa
Pliskova atakutana na Kerber kwenye mchezo wa fainali siku ya Jumatatu.
Mapema mwezi Agosti mwaka huu Serena na ndugu yake Venus Williams
walitolewa kwenye raundi ya kwanza ya mchezo wa tennis wa wanawake
wawili wawili kwenye michuano ya Olimpiki.
Serena alikuwa anatarajia kufikisha mataji 23 ya grand slam kwenye
michuano hiyo na kuvunja rekodi ya Steffi Graf ya mataji 22 ambayo
wanafanana kwa sasa.
No comments:
Post a Comment