Tuesday, 6 September 2016

Rais Magufuli aridhishwa na ujenzi wa mabweni UDSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amehidi kumalizia kiasi cha shilingi bilioni tano alichoahidi katika ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuahidi ajira kwa watendaji wa ujenzi huo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika eneo la Mlimani City ambapo kunafanyika ujenzi wa mabweni hayo ambapo amesema amefurahi kuona kuwa wakandarasi wa ndani wakijenga kwa gharama nafuu na kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia kuhifadhi wanafunzi zaidi ya 4000.

Kwa upande mwingine Dkt. Magufulli ameipongeza Wakala ya Majengo Tanzania (TBA) ambao ni wakandarasi wa ujenzi huo kwa kukubali kujenga mabweni hayo kwa gharama ya bilioni kumi ujenzi unaotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba mwaka huu na kuwataka kuwatumia vijana wanaotekeleza mradi huo katika miradi mingine.

"Hili kundi la vijana walioshiriki kufanya kazi hii msiwaache, namimi nitawapa majengo mpaka mtakimbia nyinyi wenyewe ntakuwa nikiwapa kazi, hawa vijana wamejitoa kwa nguvu zao na ndiyo wanatakeleza dhana ya hapa kazi tuu" alisema Dkt. Magufuli.

No comments:

Post a Comment