Na Sheila Simba,Maelezo.
WAKALA wa Jiolojia Nchini (GST)
imezitaka Taasisi za Umma, Wizara na Idara za Serikali kuwatumia
Wataalamu wa jiolojia katika shughuli za ujenzi wa ofisi za Serikali
Mkoani Dodoma ili kuweza kukabiliana na athari za matetemeko la ardhi
yanayotokea mara kwa mara Mkoani humo.
Wito huo umetolewa leo na
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Nchini(GST) Profesa Abdulkarim
Mruma, wakati wa mahojiano yake na MAELEZO kuhusiana na athari
zitokanakazo na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo matetemo ya ardhi
hususani katika kipindi hiki ambacho Serikali imepanga kuhamishia
shughuli zake mkoani Dodoma.
“Nashauri Serikali kutuma
wataalamu kufanya utafiti ili kuangalia ni maeneo gani yanafaa kujenga
ofisi za Serikali na zinatakiwa zijengwe kwa mfumo upi ili ziweze
kuhimili matetemeko ya ardhi pindi yanapotokea” alisema Profesa Mruma
Aliongeza kuwa hapo awali ujenzi
wa magorofa mkoani humo ilikuwa mwisho ghorofa nne kutokana na mkoa
huo kupitia na Bonde la Ufa la Afrika Mashariki ambalo kusababisha
matetemeko ya mara kwa mara.
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa
maghorofa Mkoani humo, Prof. alisema magorofa yanayotakiwa kujengwa yawe
mapana na yenye kuzingatia ugumu wa nondo, aina saruji inayotumika
katika ujenzi na uimara wa jengo husika.
“Jengo likiwa nyembamba na refu
ni rahisi kupata madhara pindi tetemeko linapotekea hivyo ni vyema watu
wafuate ushauri wa wataalamu kabla kufanya ujenzi na pia kuangalia
maeneo yanayofaa kwa ujenzi” alisema Prof Mruma
Aidha ameongeza kuwa majengo
yote yatakayojengwa yanatakiwa kuzingatia ubora wa majengo kwa kutumia
wataalamu badala ya kujenga bila kushirikisha wataalamu.
No comments:
Post a Comment