
Akizungumza wakati akipokea kivuko hicho Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kukarabatiwa kwa kivuko hicho kutapunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa Kigamboni.
Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa licha ya kukamilika kwa kivuko hicho lakini amesema serikali inaendelea kuboresha vifuko vingine katika maeneo mingine lakini pia kununua vingine vipya ila kutatua changamoto ya vivuko katika maeneo yaliyotenganishwa na maji.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa TAMESA, Le-Kjane Manase amesema kuwa wao kama wazawa wanazijivunia kukamilisha ukarabati wa kivuko hicho kwa wakati uliopangwa.
Manase amesema ukaratabati huo uliogharimu zaidi ya bilioni moja uliofanyka nchini kwa teknolojia mpya umeokoa fedha nyingi kwa kuwa marekebisho hayo hapo zamani yangeweza kufanyika, Mombasa au Afrika kusini pekee.
No comments:
Post a Comment