
Sergio Aguero
Klabu ya Manchester City imekata rufaa dhidi ya shtaka la kucheza
vibaya linalomkabili mshambuliaji wake Sergio Aguero dhidi ya mchezaji
Winston Reid kutoka West Ham.Aguero alimpiga kiwiko Winston Reid
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28,alizozana na Reid wakati wa ushindi wa 3-1 katika mechi ya ligi ya Uingereza.
Iwapo atapatikana na hatia ,mchezaji huyo wa Argentina atapigwa marufuku ya mechi tatu na kukosa deby ya Manchester mnamo tarehe 10 mwezi Septemba.
Pia ataikosa mechi ya ligi dhidi ya Bournemouth pamoja na ile ya kombe la EFL dhidi ya Swansea.
No comments:
Post a Comment