Tuesday, 13 September 2016

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula amemkingia kifua Profesa Ibrahim Lipumba

 Image result for lipumba
Jumuiya ya vyuo vikuu ya CUF, tawi la Mlimani, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), limedai kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba anatumiwa na CCM ili kukigawa.
Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula amewajia juu vijana hao akisema Profesa Lipumba ni msomi mashuhuri hapa nchini na kamwe hawezi kutumiwa kwa masilahi ya chama kingine.”

 
“Hizo tuhuma siyo za kweli, Lipumba ni profesa, msomi na amekiongoza chama hicho kwa muda mrefu. Hawezi kutumiwa, they are not fair to him (hawajamtendea haki),” alisema Mangula na kuongeza kuwa Profesa Lipumba ana heshima yake.

No comments:

Post a Comment