. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimepokea
walimu 24 kutoka Chuo cha Zhejiang Normal cha China watakaosambazwa
katika baadhi ya shule na vyuo nchini ili kujifunza Kiswahili na
kufundisha lugha yao.Akizungumza wakati wa kuwakaribisha walimu hao, Kaimu Makamu Mkuu wa UDSM (Taaluma), Profesa Florens Luoga amesema ili kuitumia fursa iliyopo ya kujifunza Kichina na kukitangaza Kiswahili duniani, kuna kila sababu ya kufurahia ujio wa wanafunzi hao.
Profesa Luoga amesema katika kuhakikisha mafunzo hayo ya lugha yanakuwa endelevu, mwakani UDSM itaanza kutoa shahada ya lugha ya Kichina.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius ya UDSM inayofundisha lugha ya Kichina, Profesa Zhang Xiaozhen amesema baadhi ya wanafunzi hao watakaa Tanzania kwa miaka miwili na wengine mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment