Tuesday, 13 September 2016

Kampuni zaidi ya 35,000 hatarini kufutiwa leseni

Zaidi ya Kampuni 35,000 ziko hatarini kufutiwa leseni na wahusika kufikishwa mahakamani kwa kutofuata sheria za uendeshaji biashara nchini Tanzania.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA), Frank Kanyusi jijini Mwanza na kusema kuwa baada ya miezi mitatu kuanzia sasa kampuni hizo zitaanza kufutwa.

Kanyusi ametoa wito kwa wanaoziendesha Kuwasilisha taarifa za kampuni zao kila siku mwaka pamoja na nakala ya mkaguzi wa fedha na kwamba kutofanya hivyo kusababisha kufungwa kwa kampuni kukiuka sheria.

Aidha aliwataka wafanyabiashara na wajasiriamali nchini Tanzania kutumia fursa ya uwepo wake kurasimisha biashara zao ili serikali iwatambue na kutoa ushirikiano katika kufanya biashara.

No comments:

Post a Comment