Chelsea wakubali kipigo wakiwa Stamford kutoka kwa Liverpool
Mchezo wa EPL uliokuwa unawakutanisha majogoo wa jiji Liverpool
dhidi ya wenyeji wao Chelsea ya London katika uwanja wao wa Stamford
Bridge katika mechi hiyo Chelsea walikubali kufungwa goli 2-1 dhidi ya
vijana wa Jurgen Klopp, Chelsea walichukua dakika 19 kuruhusu magoli
mawili yaliowafanya wakose point tatu wakiwa nyumbani, Dejan Lovren ndio
alianza kupachika goli la Liverpool dakika ya 17.
Jordan Henderson akapachika goli la pili dakika ya 36, goli pekee la
Chelsea lilifungwa na Diego Costa dakika ya 62, hii ni mara ya pili
mfululizo kwa Chelsea kuruhusu kufungwa na Liverpool katika uwanja wake
wa nyumbani kwa mechi za Ligi Kuu.
No comments:
Post a Comment