Wednesday, 5 October 2016

Ujio mpya wa Paul James Clouds


 Watafutwe wajuzi wenye kujua tafsiri za majina ya watu watueleze siri jina 'PAULO', kwa lugha iliyokuja meli ni 'PAUL'.
Matukio kadhaa ya hivi karibuni yanaonyesha watu wenye jina hilo akili zao huwaza nyumbani zaidi. Uthibitisho wa hili unapatikana Old Trafford kwenye matofali ya kuchoma; Paul Pogba aliondoka lakini sasa amerudi nyumbani. 

Hii inaonekana majina ya Paul kuwa na bahati kubwa kwa kazi wanazofanya kwa kupewa pesa nyingi wanapojiunga na kazi mpya
 
Pj alihama clouds na kuhamia EFM akiwa na rafiki yake Gerlad Hando na kufanya kipindi cha asubuhi kiitwacho Joto la Asubuhi pj ambaye kwa asilimia 80 ya kipindi cha joto alikibeba akifanya kipengele cha la mgambo na kunyamvua na kunyambulisha kwa ustadi mkubwa sana na kupelekea kipindi kupendwa sana na kufanya kipindi cha powerbreakfast cha Clouds kushuka kwa wasikilizaji


Na amerudi na kufanya kipindi kilekile alichokuwa anafanya mwanzoni katika kipengele cha kuperuzi na kudadisi akiungana na Babra Hassan Masoud kipanya na wengine

No comments:

Post a Comment