Ally Daud-MAELEZO
Mfumuko wa bei wa umeshuka kwa
asilimia 4.5 mwezi Septemba kutoka asilimia 4.9 ya mwezi Agosti mwaka
huu kutokana na kupungua kwa upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa
mwezi uliopita.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),
Bw. Ephraim Kwesigabo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo
Jijini Dar es salaam.
Kwesigabo amesema kuwa kushuka
kwa mfumuko wa bei kumetokana na kupungua kwa kasi ya upandajiwa bei za
bidhaa na huduma mbalimbali ikilinganishwa na Mwezi Agosti .
“Mfumuko wa bei mwezi Septemba
umeshuka ukilinganisha na mwezi Agosti kutoka asilimia 4.9 hadi kufika
asilimia 4.5 kutokana na kushuka kwa upandaji wa bei za bidhaa na
huduma”. Alisema Bw. Kwesigabo.
Aidha aliongeza kuwa mfumuko wa
bei za bidhaa za vyakula na vinywaji Baridi vimepungua hadi kufika
asilimia 6.0 kutoka asilimia 7.0 mwezi agosti mwaka huu.
Kwesigabo amesema kuwa ushukaji
huo wa bei za vyakula na vinywaji baridi umetokana na kupungua kwa kasi
ya bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi
kilichoisha kwa mwezi Septemba mwaka huu.
Mbali na hayo Kwesigabo amesema
kuwa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania imefikia shilingi 97.4 katika
kununua bidhaa na huduma kwa mezi septemba ikilingfanishwa na shilingi
96.83 mwezi Agosti.
Aidha Mkurugenzi Kwesigabo
amesema kuwa anawaomba wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano
wa dhati kwa Ofisi za takwimu Za Mikoa wakati wa ukusanyaji wa takwi,u
mbalimbali kwa maendeleo ya nchi yetu.
No comments:
Post a Comment