Monday, 20 June 2016

Roma Italia yamchagua mwanamke wa kwanza meya

 
Wapigaji kura katika mji mkuu wa wa Roma nchini Italia, wamemchagua mwanamke wa kwanza kuwa meya wa mji huo.
Virginia Rajji wa vuguvugu la 5 Star, amemshinda mpinzani wake Roberto Giachetti katika kura ya marudio

Bwana Giachetti, ni mfuasi wa chama cha demokrasia cha mrengo wa kati-kushoto, chake waziri mkuu wa bw Matteo Renzi, ambacho pia kilipoteza kiti cha umeya katika mji wa Turin, huku wagombea wa chama chao wakishinda viti vya umeya katika miji ya Milan na Bologna.

Virginia Rajji wa vuguvugu la 5 Star, amemshinda mpinzani wake Roberto Giachetti katika kura ya marudio.
Bi Rajji, ambaye aliendesha kampeini yake akiahidi kukabiliana na ufisadi na kuwasaidia wasiojiweza katika jamii, amesema kuwa ushindi wake ni mwanzo wa enzi mpya ya uongozi nchini Italia.

No comments:

Post a Comment