Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni alipowasili katika Gereza Kuu la Karanga, Mkoani
Kilimanjaro wakati alipotembelea kiwanda cha viatu kilichopo gerezani
haapo ili kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali hasa viatu. Naibu
Waziri huyo amelitaka Jeshi hilo kuzidi kuboresha bidhaa za viatu hivyo
ili kujipatia soko kubwa ndanni ya nchi na kutekeleza agizo la Rais
Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini yanattumia viatu
vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni akisalimiana na Mkuu wa Gereza la Karanga,
Kamishna Msaaidizi Mkwiche mkoani Kilimanjaro wakati alipofanya ziara
katikaa Kiwanda cha viatu kilichopo katika gereza hilo ili kujionea
uzalishaji wa bidhaa za viatu ambavyo Rais Magufuli alitaka majeshi
yote nchini kutumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni akisikiliza maelezo kuhusu uzalishaji wa viatu
katika kIwanda cha Gereza la Karanga kutoka kwa Fundi Mkuu wa Kiwanda
hicho Ali Jambaraga wakati alipofanya ziara yake kwenda kujionea
uzalishaji wa bidhaa mbalimbali lakini pia ametaka wazidi kuzalisha
bidhaa bora zaidi ili kuteka soko la ndani na je ya nchi ikiwa ni pamoja
na kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini
kutumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni akijionea kiatu aina ya Safari buti
kinachozalishwa na Kiwanda cha Karanga kilichopo Mkoani Kilimanjaro
wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja kiwandani katika Mkoa
huo. Masauni amesisitiza kiwanda hicho kuzalisha bidhaa bora zaidi ili
kuteka soko kubwa zaidi pamoja na kutekeleza agizo la Rais Magufuli
kuhakikisha majeshi yote nchini yanatumia viatu vinavyozalishwa na Jeshi
hilo. Kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho Mrakibu Msaidizi, Michel Minja na
kushoto ni Ali Jambaraga Fundi Mkuu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni akiangalia kiatu kilichokuwa tayari kuvaliwa
kilichotengenezwa katika kiwanda cha Karanga kilichopo Gereza Kuu la
Karaga mkoani Kilimanjaro. Naibu Waziri huyo amesisitiza Jeshi hilo
kuzidi kutengeneza bidhaa bora zaidi za viatu ili kuhakikisha wanapata
soko kubwa ndani nan je ya nchi., kulia ni Kamishan Msaidizi Mwandamizi
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa aliye aambatana nae kwenye
ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masaun (aliyevaa koti) akitoa maelekezo kwa Wakuu wa Gereza
la Karanga na kiwanda cha Viatu kilichopo gerezani hapo. Masauni
amelitaka jeshi hilo kuzidi kutoa bidhaa bora ili kuendelea kuteka soko
kubwa ndani nan je ya nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
nchi, Hamad Masauni, (mwenye tisheti nyekundu) akielekea kutizama mpaka
wa Tarekea wilayani Rombo ili kujionea changamoto zinazotokana na
mipaka hiyo pamoja na kutoa maagizo kwa viongozi wanaohusika kuimarisha
ulinzi wa mpaka huo ili kukabiliana na upitishaji wa bidhaa za magendo
pamoja na wahamiaji haramu ambao wamekua wakiinia nchini bila vibali. Wa
kwanza kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimaanjaro Kamishna
Msaidizi Mwandamizi Wilbrod Muutafungwa akifatiwa na Kamishna wa
Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Mwanguku, na wan ne kutokea kulia ni Mkuu
wa Wilaya ya Rombo Agnes Hokororo alieambatana na Naibu Waziri huyo
kuangalia mipaka hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishna
Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimajaro alipotembela mpaka wa Tarakea
wilayani Rombo Naibu waziri Masauni amesema kuwa licha ya changamoto
zinazojitokeza katika mipaka yote miwili ni lazima kuendelea kuimarisha
ulinzi kwenye mipaka hiyo na kudhibiti njia zote zisizo rasmi
zinazotumiwa na wahamiaji haramu pamoja na wafanyabiashara za magendo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masaun akipewa maelezo na Afisa Mipaka Holili Michel Amo,
juu ya jiwe linaloonyesha mpaka wa Tanzania na Kenya lililopo katika
mpaka wa Holili ambalo limekua likisogezwa na watu wasiojulikana hivyo
kuharibu alama za mipaka. Naibu waziri Masauni amesema kuwa licha ya
changamoto zinazojitokeza katika mipaka yote miwili ni lazima kuendelea
kuimarisha ulinzi kwenye mipaka hiyo na kudhibiti njia zote zisizo rasmi
zinazotumiwa na wahamiaji haramu pamoja na wafanyabiashara za magendo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masaun aagiza Jeshi la Magereza kuzidi kuboresha viatu
vinavyotengenezwa na kiwanda chao ili kujipatia soko kubwa ndani ya nchi
na nje.
Hayo aliyasema jana kwa wakuu wa
Gereza la karanga na viongozi wa kiwanda hicho alipofanya ziara yake ya
siku moja katika kiwanda cha viatu kilichopo katika gereza hilo, mkoani
Kilimanjaro
Aidha, Naibu Waziri huyo
alisisistiza Jeshi hilo kutekeleza agizo la Rais John Magufuli
kuhakikisha majeshi yote nchini yanatumia viatu vinavyozalishwa na Jeshi
la Magereza, hivyo ni muhimu kuendelea kuzalisha bidhaa zilizo bora
zaidi
Haiingii akilini maofisa wa
majeshi mbalimbali nchini kuagiza viatu nje ya nchi wakati viwanda vya
ndani vinauwezo wa kuzalisha viatu bora zaidi vinavyodumu kwa muda mrefu
kuliko vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi, alisema Masauni.
Masauni alisema kwamba dhamira ya
Serikali ya awamu ya tano ya kuipeleka nchi katika uchumi wa kati hivyo
Jeshi la Magerezaa kupitia kiwanda chake na miradi mingine mingi halina
budi kuendelea kuzidisha kuzalisha viatu bora vitakavyo kidhi kiwango
cha uhitaji na soko ili kukuza uchumi wao na Serikali kwa ujumla.
Aidha, katika ziara yake, Naibu
Waziri Masauni amesisitiza kuwa ni muhimu Jeshi hilo kufanya miradi
mingi kwa ustadi mkubwa ili kujipatia psa zitakazosaidia kujiendesha wao
kama jeshi na mashirika mengine yanayounga mkono miradi yao hivyo
kutotegemea ruzuku kutoka serikalini.
Waziri huyo alilipongeza Jeshi
hilo kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora kulinganisha na nyingine
zinazoingizwa nchi, hivyo amesisitiza kuzidi kutengeneza viatu bora
zaidi ili kuwa na uwanja mpana wa soko la ndani nan je ya nchi.
No comments:
Post a Comment