Hamisi
Maduka Kaimu mwenyekiti wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani
Tabora akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha
Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alisistiza ulipaji wa fidia za
Ardhi uzingatie uhalisia wa thamani ya eneo husika.
Abdallah
Moto mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa
maoni yake kwa Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya
Ardhi ya 1995 kuhusu suala la kupewa kipaumbele utoaji wa hati miliki
kwa wanavijiji.
Shakira
Masudi mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa
maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya
Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alitaka Sera itambue wamiliki wa Ardhi wa
maeneo wa muda mrefu katika kutoa Hati.
Mwl.
Hadija Nyembo mkuu wa wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora akisisitiza jambo
mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi
ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora.
Hanifa
Selengu Mkuu wa wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora akisisitiza jambo
mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi
ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Ardhi.
Na Mwanahiba Said
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la ukusanyaji wa maoni na kuipitia
upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kuiboresha. Zoezi hilo limeanza
Mwaka huu wa 2016 ambapo linashirikisha kanda nane za Ardhi ambazo ni
Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kusini, Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda
ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.
Na kwa sasa kamati maalumu ya
kukusanya maoni ipo mkoani Tabora ikikusanya maoni ya wananchi na wadau
mbalimbali wa sekta ya Ardhi ili kupata sera iliyoridhiwa na wengi.
Katika sekta ya Ardhi Serikali ya
Tanzania imekuwa ikitekeleza Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 kwa
takribani miaka 20 hadi sasa, hata hivyo zimejitokeza changamoto nyingi
ambazo zinalazimu kufanya mapitio ya sera hiyo.
Migogoro na malalamiko
yanayotokana na ardhi ni changamoto zinazo chukua nafasi kubwa katika
jamii yetu na imekuwa ikiigharimu kwa kiasi kikubwa katika kuitatua.
Kuongezeka kwa migogoro hii
imekuwa ni changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi pamoja na watumiaji
mbalimbali wa ardhi hususan wakulima na wafugaji, wawekezaji, wananchi,
vijiji na hifadhi.
Hata hivyo, kuongezeka kwa
mahitaji ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji hususan katika sekta za kilimo,
madini, viwanda na wananchi kutonufaika na uwekezaji unaofanywa katika
ardhi na hivyo kusababisha migogoro baina ya wananchi na wawekezaji.
Aidha kutokuwepo kwa mipango ya
matumizi endelevu ya ardhi mijini na vijijini na hata sekta ya ardhi
kuvamiwa na madalali ni changamoto iliyoifanya Serikali kuamua kuipitia
upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995.
Changamoto zote kwa pamoja,
zimelazimika kufanyika kwa mapitio ya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili
kutoa mwelekeo mpya na usimamizi wa ardhi kwa manufaa ya watanzania
wote.
Ardhi ni Sekta mama na hivyo basi
Sera ya ardhi ni sera mama katika masuala yote ya Maendeleo ikiwemo
kilimo na mifugo, ambayo shughuli zake zinafanyika kwenye ardhi.
Na sasa Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la ukusanyaji wa Maoni na kuipitia
upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kuiboresha. Zoezi hilo limeanza
Mwaka huu wa 2016 ambapo linashirikisha kanda nane za Ardhi ambazo ni
Kanda ya Dar es Salaam, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kusini, Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda
ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment