Wednesday 25 May 2016

Taliban wamteua Kiongozi Mpya


Mullah

Mullah Mansour aliuawa Jumamosi
Kundi la wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan limemteua kiongozi mpya baada ya kuuawa kwa Mullah Mansour.
 
Bw Mawlawi Haibatullah Akhundzada ndiye kiongozi mpya.
Manaibu wake watakuwa Sirajuddin Haqqani, ambaye mtandao wake umedaiwa kutekeleza mashambulio mengi ya mabomu Kabul, na Mohammad Yaqoob, mwanawe mwanzilishi wa Taliban, Mullah Omar.
Mansour aliuawa katika mkoa wa Balochistan nchini Pakistan kwenye shambulio lililotekelezwa na ndege za Marekani zisizokuwa na rubani.
Rais wa Marekani Barack Obama Jumatatu alithibitisha kifo cha Mansour Jumatatu.
  • App ya simu ya Taliban yatolewa sokoni
Pentagon ilisema Mansour amekuwa akipanga mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.
Taliban
Wapiganaji wa Taliban wamekuwa wakitekeleza mashambulio Afghanistan na Pakistan
Jumanne, waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan Chaudhry Nisar Ali Khan aliambia wanahabari kwamba mwili wa Mansour ulipatikana karibu na mpaka wan chi hiyo na Pakistan.

No comments:

Post a Comment