Monday 30 May 2016

Bungeni leo yaliojiri leo



 Mbunge wa jimbo la Ukonga (CHADEMA) Mhe. Mwita Mwikwabwe akisoma kitabu cha Kanuni za Kudumu za Bunge ndani ya Ukumbi wa Bunge. 

 
  Mbunge wa Nzega Mhe. Hussein Bashe (CCM) akizungumza jambo na Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kulia) nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha 32 cha mkutano wa tatu wa Bunge leo mjini Dodoma.

 
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari Barbro Johansson iliyoko jijini Dar es salaam wakiondoka ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Sulemani Jafo akijibu maswali ya wabunge yaliyoelekezwa kwenye wizara yake Bungeni mjini Dodoma.
 Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge kufuatia Naibu Spika wa Bunge hilo Mhe. Tulia Ackson kutangaza kuliahirisha Bunge leo mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba nje ukumbi wa Bunge.
 Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akizungumza jambo na wabunge leo mjini Dodoma.
 Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
  Mbunge wa Kigoma Mhe. Peter Selukamba akijadiliana jambo na  Mbunge wa Nzega mjini Mhe. Hussein Bashe (kushoto)Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu nje ya Ukumbi wa Bunge mjini.
Kikao cha 32 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asubuhi.
 Wabunge wakiondoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya Naibu Spika kutangaza kuahirisha shughuli za Bunge leo.
 Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment