Tuesday 31 May 2016

Raymond WCB alishiriki kuandika nyimbo ya AY Zigo



Raymond ni msanii mwenye vipaji vingi vilivyomvutia Diamond amsainishe kwenye label yake, WCB.
Miongoni mwa vipaji alivyonavyo ni uandishi wa nyimbo huku akiwa ameshiriki kuandika hits kadhaa zikiwemo za bosi wake, Diamond.  Ray alisema bosi wake ni mtu anayependa sana 


kushauriana na watu mbalimbali ili kupata kitu kizuri na ndio maana alimpa nafasi kijana wake ampe melody na mistari kadhaa kwenye verse ya remix ya Zigo ya AY.

“Yeye ni msanii wa melody za kulalamika sana kwahiyo alivyosikia ile beat ina uchizi flani, kuna baadhi ya melody kama ile mukide mukide nikamuambia tukiweka hapa inakaaje, yeye anatafuta maneno,” alisema Ray.

Amesema pia alishiriki kutoa idea zake kwenye Make Me Sing. Lakini amedai kuwa bosi wake pia ameshiriki kumpa maneno mengi na melody kwenye wimbo wake Kwetu. Pia amedai kuwa Harmonize naye amechangia ideas zake kwenye wimbo wake Natafuta Kiki.

Kwa upande mwingine Ray alishirikiana an Dogo Janja kuandika wimbo wake My Life.
Akizungumzia boss wake, Ray amesema Diamond ni msanii anayeishi maisha simple kuliko watu wanavyoweza kudha

No comments:

Post a Comment