Thursday 26 May 2016

Serikali imewapa miezi miwili wananchi waishio katika kijiji cha michezo cha Changamani

CH1Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akitoa agizo la kuhama kwa wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam(Hawapo Pichani) kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.
 
CH2Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisistiza jambo mbele ya wajumbe wa kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.
CH3Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya akichangia hoja katika kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.
CH4Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw.Mafuku Rajabu akifafanua jambo katika kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.
CH5Eneo la Changamani kijiji cha Michezo ambalo wananchi wake wanatakiwa kuhama ndani ya miezi miwili kupisha uendelezwaji wa eneo hilo kwa ajili ya michezo mbalimbali.
Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM

Na Chrispino Mpinge
Serikali imewapa miezi miwili wananchi waishio katika kijiji cha michezo cha Changamani kilichopo Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam  kuhama katika eneo hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha mchezo.


Agizo hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipokutana na wananchi hao katika kikao cha kujadili na kukubaliana muda wa kuhama katika eneo hilo leo Jijini Dar es Salaam.
“Ndugu zangu tumejadiliana wote na kukubaliana kuwa baada ya miezi miwili mtakuwa mmeshaama katika eneo hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha michezo kwa ajili ya shughuli za mbalimbali za michezo” alisisitiza Bw. Nkenyenge.

Naye Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw.Julius Mgaya amesema kuwa mpango wa kuwahamisha wananchi hao unalenga kutekeleza mradi wa kijiji cha michezo kitakachojengwa kwa ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali.

Kwa upande wake mmoja ya wawakilishi wa wananchi hao Bw.Atillio Mballa amesema wamekubaliana na muda huo waliopewa na watafikisha ujumbe huo kwa wenzao na kabla ya muda hujafika watakuwa wameshatekeleza agizo hilo.
Katika mpango wa kukuza na kuendeleza michezo nchini Serikali imejipanga kukuza sekta ya michezo nchini na kuifanya kuwa moja ya rasilimali itakayochangia katika pato la taifa.

No comments:

Post a Comment