Mwanamuziki wa
taifa la Benin aliyeshinda tuzo ya Grammy Angelique Kidjo, pamoja na Wanaharakati 3 kutoka barani Afrika wametuzwa tuzo ya haki za
kibinaadamu mwaka 2016 kwa kusimamia haki na shirika la Amnesty
International.
Wote wameonyesha kwamba wanapigania haki za kibinaadamu kwa kutumia vipaji vyao kuwashiwishi wengine, Salil Shetty katibu mkuu wa Amnesty International amesema katika taarifa.
Kidjo pia anajulikana kwa kampeni yake kwa uhuru wa kujieleza pamoja na vita dhidi ya Ukeketaji.
Mwanamuziki huyo amejiunga na orodha ya watu maarufu ambao wameshinda tuzo ya Ubalozi wa watu walio na dhamira ya kubadilisha uovu katika jamii ,akiwemo rais wa kwanza Afrika kusini Nelson Mandela na msanii wa China Ai Weiwei.
No comments:
Post a Comment