Mchezaji wa soka ya kimataifa kutoka Cameroon, Patrick Ekeng, amefariki baada ya kuanguka uwanjani katika ligi ya Romania.
Hakuwa amegusana wala kukaribiana na mchezaji mwingine alipoanguka uwanjani.
Matabibu walimkimbiza hospitalini ambako madaktari walijaribu kumfufua kwa zaidi ya saa Moja bila kufaulu.
Kwa muda wa miaka michache iliyopita wachazaji kadhaa Waafrika wamefariki walipokuwa wakicheza uwanjani.
No comments:
Post a Comment