Monday, 2 January 2017

Shule ya Umwani ya CCM yachukuliwa na Serikali

Image result for magufuli bukoba
"Bahati nzuri au bahati mbaya mimi ndiye Mwenyekiti wa CCM, natambua ile shule ya Umwani ni ya CCM, sasa naagiza iwe ya Serikali.
Na Profesa Ndalichako yupo hapa ahakikishe masaula yote pamoja na madai ambayo shule wanadaiwa na Jumuiya ya Wazazi yalipwe na shule irudishwe serikalini.
Walimu na Wanafunzi wote watabakia pale pale na watakuwa ni wa serikali wawe wameshindwa au kushinda mitihani yao." Rais Dk Magufuli, Bukoba.
Hayo ni maneno ya Rais Magufuli mapema leo Januari 2, 2017 alipokuwa akiongea na wakazi wa Bukoba ikiwa ni sehemu ziara ya siku mbili mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment