Wednesday 25 January 2017

Mtu mrefu aendesha gari akiwa amesimama

 Ashtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amesimama
Mtu mrefu ameshtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amesimama baada ya kukiri kupeleka gari vibaya.
Adam Elliott alituhumiwa kwa kuwaonyesha madereva wengine kichwa chake kikiwa kinaonekana juu ya paa la gari hilo aina ya Ford Ka.
Elliott mwenye umri wa miaka 26 kutoka mji wa Newcastle, ambaye ana urefu wa mita mbili alikiri kufanya makosa hayo katika mahakama ya Newcastle lakini akalaumu urefu wake.

Adam Elliott
Akizungumza baada ya kesi hiyo, alisema: Sikuwa nimesimama, mimi ni mrefu ndio maana.
Jaji Robert Adams alisema kuwa ni wazi kwamba Adam alitaka kuonekana akiendesha gari akiwa amesimama ili kuonyesha urefu wake.
''Ilikuwa kitu hatari sana kufanya'',alisema.

No comments:

Post a Comment