Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TABD) Bw. Francis Assenga akizungumza na
waandishi wa habari leo Jijini Dar es saalam kuhusu mikakati ya Benki
hiyo kuwainua wakulima wadogo ili waweze kushiriki katika ujenzi wa
uchumi wa viwanda. Kushoto ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa
Benki hiyo, Bw. Albert Ngusaru.
Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TABD) Bw. Francis Assenga akizungumza na
waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam ambapo alibainisha kuwa
Benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo kwa wakulima ili kuziba pengo la
upatikanaji wa fedha kwenye minyororo ya thamani katika sekta za kilimo,
mifugo, uvuvi na mazao ya misitu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo
na Biashara Bw. Geofrey Mtawa na kushoto Mkurugenzi wa Hazina na
Utafutaji Fedha Bw. Albert Ngusaru.
Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo na
Biashara Bw. Geofrey Mtawa akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu mpango
wa Benki hiyo kuhakikisha kuwa wakulima wote wanawezeshwa ili kuinua
kilimo hapa nchini. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo (TABD) Bw. Francis Assenga.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania leo Jijini Dar es salaam.
(Picha na Frank Mvungi- Maelezo)
No comments:
Post a Comment