Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa
wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM
Profesa Bertha Omari Koda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono akiwaonyesha
waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu kinachotumika kutoa elimu
juu ya usawa wa kijinsia katika sekta ya kilimo, sheria za kimila leo
jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mhadhiri wa Shule Kuunya
Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) Bw. Dotto Kuhenga,
Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari
Koda na Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na
Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele.
Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma
ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari wakati wa mkutano wao na waandishi hao(hawapo
pichani) kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo,
uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES
Dkt. Rose Kingamkono na Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala
Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (Sehemu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma –SJMC) Bw,
Dotto Kuhenga akionyesha waandishi wa habari kitabu cha mwongozo wa
waandishi wa habari katika utekelezaji wa mradi wa uhamasishaji usawa
wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la
Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono na Mtafiti kutoka Taasisi
ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda (kulia).
Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya
Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth
Henjewele akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa
kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la
Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono.
No comments:
Post a Comment