Meneja wa kanda ya kaskazini wa
Benki ya KCB Tanzania Judith Lubuva, akiongea na wanawake wajasiriamali
waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani
Arusha.
Afisa Mawasiliano ya Umma wa
benki ya KCB Margaret Makere akiongea na wanawake wajasiriamali
waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hiyo mkoani
Arusha.
Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo
cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Nina Nchimbi akitoa mafunzo
ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake
wajasiriamali wa mkoa wa Arusha.
Meneja wa kanda ya kaskazini wa
Benki ya KCB Tanzania Judith Lubuva (aliyekaa wapili kulia) akiwa kwenye
picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali waliohudhuria na kumaliza
mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na benki hiyo katika mkoa wa Arusha.
Katika swala zima la kumkomboa
mwanamke mjasajiriamali, Benki ya KCB Tanzania inaendelea na programu ya
mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali yanayoitwa 2JIAJIRI.
Programu hii inalenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika
changamoto zinazosababisha biashara yake ishindwe kuendelea.
Benki ya KCB imepanga kufundisha
wanawake wajasiriamali 315 kutoka mikoa ya Dar Es salaam, Mwanza,
Morogoro, Arusha, Moshi na Zanzibar ambapo matawi ya benki hiyo yapo.
Mafunzo haya ni bure kabisa,
benki ya KCB inagharimia gharama zote. na yanahusisha Elimu ya Fedha
(Financial Literacy), Kufikiwa huduma za kifedha (Financial Inclusion),
Masuala ya Kisheria (Legal Framework), Ushindani wa Kibiashara (Business
Competitiveness) na kuwa na sifa za kukopesheka (How to be bankable).
Zaidi ya mafunzo hayo, benki ya
KCB itawapatia wanawake wajasiriamali hao maafisa watakao wafundisha kwa
vitendo kwenye maeneo ya biashara zao. Maafisa hao watakua ni afisa
fedha, afisa sharia na afisa masoko.
Kwako mwanamke mjasiliamali “JIULIZE KWANINI uhangaike wakati benki ya KCB tupo!”
No comments:
Post a Comment