Monday, 2 January 2017

Asha Baraka aeleza kilichoua muziki wa dansi

Asha Baraka
 Mkurugenzi na mmliki wa bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini Twanga Pepeta, Asha Baraka ametoa malalamiko kwa vyombo vya habari Tanzania kutotoa nafasi ya kutosha 'kupromoti' muziki wa dansi na kusema hiyo ni sababu mojawapo ya muziki huo kupotea.
Akiongea na eNewz Asha Baraka alisema miongoni mwa mambo mengine yanayokwamisha muziki wa dansi ni pamoja na wanamuziki wa dansi kuwa wakilazimishwa kufanya muziki bongo fleva.
Je, kukosa ubora kwa video za wasanii wa muziki wa dansi haiwezi kuwa sababu ya muziki huo kutopewa nafasi ambayo bongo fleva inapewa katika Media?  Asha Baraka anasema “Wasanii wa dansi waanze kwanza kufanya nyimbo nzuri kama zamani, maana kwa sasa wamekata tamaa hivyo hawafanyi kazi nzuri. Halafu baada ya hapo ndiyo tuanze kufanya juhudi za kuboresha video zetu”
Na mwisho Asha alisema anaamini wizara yenye dhamana na maswala ya burudani itafanya juhudi za kusaidia kuurudisha muziki wa dansi katika chati kwa mwaka 2017

No comments:

Post a Comment