Askofu wa Dayosisis ya
Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Dk. Alex Malasusa akiweka fedha mara baada ya kuzindua tawi jipya la
benki ya Maendeleo la Kariakoo, jijini Dar es Salam, nyuma yake ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ibrahim Mwangalaba akifuatiwa na
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Amulike Ngeliama (kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa
Maendeleo Banki Ibrahim Mwangalaba akiteta jambo na baadhi ya wateja wa
kwanza waliyohudhuria ufunguzi wa tawi jipya la Kariakoo.
Askofu wa Dayosisis ya Mashariki
na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex
Malasusa akiweka wakfu na kuzindua tawi jipya la Maendeleo banki,
Kariakoo wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi, Amulike
Ngeliama, na kushoto ni Mkuu wa Jimbo la Kati Mch. Frank KImambo
Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa tawi la Kariakoo.
Baadhi ya Viongozi wa Maendeleo
Bank wakiwa katika picha ya pamoja watatu kutoka kushoto ni Meneja wa
Tawi Nuru Shadrack katika uzinduzi uliofanyika Kariako na kuzinduliwa na
Baba Askofu Dkt Alex Malasusa.
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Askofu wa Dayosisis ya
Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Dk. Alex Malasusa amezindua Maendeleo Bank Kariakoo jijini Dar es salaam
huku akitoa pongezi kwa watumishi wa Kanisa kwa kuweza kuamua
kuwasaidia Watanzania katika kuweka pesa zao katika bank hiyo.
Akizungumza na waandishi wa
habari pamoja na wadau mbalimbali waliohudhulia uzinduzi huo Askofu
Dkt.Alex Malasusa,amesema kuwa ni wakati wa Watanzania kuacha kufisha
pesa nyumbani na kuweka kwenye vibubu kwani bank hii itaweza kuwasaidia
katika kazi zao pindi wanapokuja kuweka pesa au kuomba mkopa.
“Hii Maendeleo bank ni ya watu
wote haichague dini kwa hiyo mtu yoyote anweza kufungua Account kwa
lengo la kutunza pesa zao na pia amewaasa watanzania kuwa na nidhamu ya
pesa kwani wataweza kufanya shughuli zao kwa kufuata misingi ya dini
pamoja na sheria za nchi”amesema Askofu Dkt.Alex Malasusa
Kwa Upande wa Mkurugenzi
Mtendaji Mr.Ibrahim Mwangaleba amesema kuwa Maendeleo bank ni ya watu
wote wa dini zote na inawakaribisha wateja waje kuweka pesa zao katika
mahali salama na haitakuwa na ubanguzi wowote japokuwa ni ya Kikristo.
“Sisi tumeamua kufungua tawi la
Maendeleo bank katika eneo la Kariakoo na tunaamini kwa imani kuwa hii
itakuwa bank kubwa kuliko tawi lolote hapa jijini Dar es salam na
itakuwa bega kwa bega na wateja watakaokuja kuchukua mkopo kwani hapa
Fedha zitakuwa na maombi kwa lengo la wateja kwenda kuwa na maendeleo ya
hali ya juu”amesema Mwangaleba
No comments:
Post a Comment