Monday 30 January 2017

Rais Trump atetea hoja yake kuhusu Wanaotaka kuingia Nchini Marekani

Rais Trump atetea hoja yake kuhusu usafiri 
Rais wa Marekani Donald Trump ameteta marufuku yake ya muda ya kusafiri kwa watu wanaotoka nchi saba alizoorodhesha.
Rais Trump amewalaumu waandishi wa habari kwa kuupoteza umma baada ya kusema sera hiyo imelenga nchi za Kiislamu peke yake.

Kwa mujibu wa habari Rais Trump amesema viza zitatolewa kwa wasafiri kutoka nchi zote ndani ya siku tisini.
Hata hivyo kiongozi wa wafanyakazi wa Serikali Reince Priebus amesema marufuku hiyo haitawahusu wenye kuhodhi kadi za Green ambao wana haki ya kisheria kuishi Marekani.
Sera hii imeonekana kupingwa vilivyo na nchi nyingi.

No comments:

Post a Comment