Misikiti mikubwa minne nchini Uholanzi yafungwa kwa muda baada ya tukio la shambulizi la msikiti mjini Quebec nchini Canada .
Kwa mujibu wa shirika la habari la Uholanzi ni kuwa baada ya shambulizi
la Canada maafisa wakuu wa misikiti hiyo minne walifanya mkutano wa
dharura .
Baadaye misikiti hiyo mikubwa iliyopo katika miji ya Amsterdam,
Rotterdam, Hague na Utrecht ilitangazwa kufungwa kwa muda na kwa ajili
ya usalama .
Takriban watu 6 walifariki baada ya watu 3 kuingia katika msikiti mmoja
Canada na kushambulia waumini waliokuwa wanafanya sala ya usiku ,8
wameripotiwa kujeruhiwa katika shambulio hilo .
No comments:
Post a Comment