Monday, 30 January 2017

Obama anaweza kulipwa hadi shilingi bilioni 99 kuandika kitabu kipya cha maisha yake

Barack Obama amepumzika sasa baada ya kuitumikiaa Marekani kwa miaka minane kama Rais. Lakini, hiyo haimaanishi kuwa ametoka kwenye mzunguko wa fedha. Na tena, huenda akaanza kuingiza nyingi zaidi, asante kwa mikataba minono inayomuwinda kutoka kwa wachapishaji wa vitabu.

Yeye na mkewe Michelle, ni uamuzi wao tu, kukubali kusaini mikataba ya vitabu, yenye thamani ya kuanzia dola milioni 20 hadi 45. Fedha hizo, pamoja na matumizi mengine, zitamwezesha kugharamikia bili za ndege binafsi, sababu amewahi kudai kuwa hatopenda kusafiri na ndege za kawaida akistaafu.

Kwa mujibu wa New York Times, mawakala wa masuala ya vitabu wanadai kuwa Obama ana nafasi ya kuandika kitabu chenye thamani kubwa zaidi kuwahi kuandikwa na Rais yeyote.
Wengine wanadai kuwa Obama anaweza kuingiza zaidi ya dola milioni 12, na mkewe zaidi ya dola milioni 10.

Obama amewahi kuandika vitabu vitatu, “Dreams From My Father,” “The Audacity of Hope” na “Of Thee I Sing” ambavyo vimeuza zaidi ya nakala milioni 4 duniani na kumuingiza zaidi ya dola milioni 10.

No comments:

Post a Comment